Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga

Wakati mashabiki wa Yanga wakisubiri utambulisho wa kocha mkuu anayetua kuchukua nafasi ya Manqoba Mngqithi, kuna uwezekano mkubwa kwa Kocha Msaidizi Simon Dladla akaendelea kuwa sehemu ya benchi la ufundi akiwa kocha msaidizi.

Dladla alikabidhiwa majukumu ya kaimu kocha mkuu na amefanya vyema katika mechi mbili alizokaa kwenye benchi la ufundi.

Aliiongoza Yanga kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa Fc na kisha kuwaongoza tena Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mechi hizo halikuwa suala la ushindi tu, pia yalionekana maboresho makubwa ya kimbinu, timu ikishambulia kwa kasi huku uwajibikaji wa wachezaji ukionekana.

Dladla ameonyesha uwezo wake na pengine hilo linatosha kumbakisha katika benchi la ufundi.

Kinachosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa yanga ni kutangazwa jina la kocha mkuu ambaye huenda akaendelea na sehemu kubwa ya wataalam waliopo sasa kwenye benchi la ufundi.

Nafasi nyingine inayosubiri kujazwa ni ya kocha wa viungo baada ya Chyna Mokaila kupewa mkono wa kwaheri sambamba na Manqoba.

Kwa sasa uongozi wa Yanga umewapa wachezaji mapumziko ya siku chache kabla kurejea kuanza maandalizi ya mechi zitakazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Happy Birthday Mwamnyeto
Happy Birthday Mwamnyeto
2h ago
READ MORE β†’
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
5h ago
READ MORE β†’
Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL
Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL
17h ago
READ MORE β†’
Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
23h ago
READ MORE β†’
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
1d ago
READ MORE β†’
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
1d ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
2d ago
READ MORE β†’