Usiku wa kuamkia leo Yanga imemthbiitisha rasmi kocha wake mpya Fadlu Davids anayetua kurithi mikoba iliyoachwa na raia mwenzake wa Afrika Kusini, Manqoba Mngqithi.
Yanga imemuajiri Fadlu baada ya mpango wa awali wa kumpata kocha Sead Ramovic kukwama dakika za lala salama.
Fadlu ni kocha mwenye uzoefu na soka la Tanzania hivyo tayari anafahamu ukubwa wa jukumu lililopo mbele yake.
Kwa mashabiki wa Yanga jambo muhimu kwa sasa ni kumuunga mkono kocha huyo mpya.
Ni mapema sana kuhukumu wakati hata hawafahamu kile anachokwenda kuifanyia timu yao.
Jambo lla uhakika ni kuwa Fadlu anafahamu ugumu wa kazi iliyo mbele yake.
Karibu Jangwani Fadlu..!
ADVERTISE HERE