Kikosi cha Yanga kimewasili visiwani Zanzibar tayari kwa kambi maalum ya siku 10 katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA.
Kocha Mpya wa Yanga Fadlu Davids ameongoza msafara wa timu hiyo akiwa tayari kuanza majukumu yake.
Baada ya kutambulishwa rasmi, Fadlu sasa atakuwa na siku 10 muhimu za kukiweka sawa kikosi chake kabla ya kurejea kwa ligi na kufuatiwa na mechi za hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.
Mashabiki wa Yanga wanasubiri kuona timu yao ikiwa imara zaidi baada ya kambi hiyo visiwani Zanzibar.




ADVERTISE HERE