Baada ya kuanza kazi Yanga, milio inasikika upande wa pili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30m ago
Baada ya kuanza kazi Yanga, milio inasikika upande wa pili

Kocha Mkuu wa Yanga Fadlu Davids jana ameongoza rasmi mazoezi ya kwanza ya kikosi cha Wananchi kilichoweka kambi Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Hata hivyo haikuchukua muda mrefu milio kusikika kutoka kwa watani zao upande wa pili baada ya klabu ya Simba kufungua madai FIFA dhidi ya Fadlu wakimtuhumu kuvunja mkataba na klabu hiyo kinyume cha taratibu msimu uliopita.

Fadlu aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita na kujiunga na klabu ya Raja CA baada ya Morocco. Aliondoka Simba baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United uliopigwa huko Botswana.

Hata hivyo hakukuwa na malalamiko yoyote kutoka kwa Simba dhidi ya Fadlu katika kipindi chote alichokuwa anaitumikia Raja CA lakini baada ya kutua Yanga mambo yamebadilika.

Kwa mujibu wa taarifa, kesi baina ya pande hizo imepangwa kusikilizwa Januari 2027 na Shirikisho la soka duniani (FIFA).

Kwa upande wa Fadlu amewaachia Wanasheria wake kushughulikia kesi hiyo huku yeye akijikita kwenye majukumu yake na Yanga.

Fadlu ameanza majukumu yake akiwa na ari kubwa akipania kuirejesha Yanga kwenye makali yake baada ya kuyumba mwanzoni mwa msimu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 09 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 09 2026
1h ago
READ MORE β†’
Siku 10 za kuisuka upya Yanga Zanzibar
Siku 10 za kuisuka upya Yanga Zanzibar
20h ago
READ MORE β†’
Dladla ataendelea na majukumu ya Kocha Msaidizi Yanga
Dladla ataendelea na majukumu ya Kocha Msaidizi Yanga
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 08 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 08 2026
1d ago
READ MORE β†’
Fadlu atua Avic Town, kuweka mipango sawa
Fadlu atua Avic Town, kuweka mipango sawa
1d ago
READ MORE β†’
Fadlu aongeza wawili benchi la ufundi Yanga
Fadlu aongeza wawili benchi la ufundi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Nimefurahi kujiunga na Yanga - Fadlu
Nimefurahi kujiunga na Yanga - Fadlu
2d ago
READ MORE β†’
Kazi ndio inaanza, Fadlu ni rasmi
Kazi ndio inaanza, Fadlu ni rasmi
2d ago
READ MORE β†’
Fadlu alivyotua, ujumbe wake kwa Wananchi
Fadlu alivyotua, ujumbe wake kwa Wananchi
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
2d ago
READ MORE β†’