Baada ya mazoezi ya takribani siku sita, kikosi cha Yanga chini ya kocha Fadlu Davids kesho Jumamosi kitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki visiwani Zanzibar.
Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya KVZ katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Maisara.
Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 12 jioni.
Huo utakuwa mchezo wa kwanza w kujipima kwa Fadlu tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa Yanga akichukua majukumu yaliyoachwa na Manqoba Mngqithi.