Wakati Yanga ikiendelea kuwakosa Mohamed Mussa, Hussein Masalanga na Maxi Nzengeli kutokana na majeraha, jana Ibrahim Bacca na Albert Kangwanda waliumia wakiwa kwenye majukumu ya timu za Taifa.
Bacca alipata majeraha kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2027 dhidi ya Nigeria huku Kangwanda akiumia kwenye mchezo dhidi ya Burundi.
Hata hivyo taarifa za awali zimebainisha kuwa nyota hao hawakupata majeraha makubwa sana wakisubiri uchunguzi zaidi.
Sio habari nzuri sana kwa mashabiki wa Yanga hasa katika kipindi hiki kuelekea kipindi muhimu cha mechi za hatua ya makundi CAFCL.
Ni hivi karibuni tu Dickson Job na Clement Mzize walirejea kikosini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu huku Duke Abuya na Yao Kouassi nao wakianza mazoezi ya timu baada ya kukosekana uwanjani kwa takribani wiki tatu.