Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19h ago
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20

Baada ya takribani wiki tatu za mapumziko ya kalenda ya FIFA, mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi tatu kupigwa.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga wako mkoani Kilimanjaro ambapo majira ya saa 10 jioni watashuka uwanja wa Ushirika kuikabili Polisi Tanzania.

Kikosi cha Yanga kiliwasili Moshi jana usiku tayari kwa mtanange huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Ni mchezo unaozikutanisha timu mbele zenye safu bora za ushambuliaji kwenye ligi.

Kinara wa mabao mpaka sasa msimu huu ni Anuary Jabir mshambuliaji wa Polisi Tanzania aliyefunga mabao saba akifuatiwa na Peter Shalulile wa Yanga aliyefunga mabao sita.

Kwenye msimamo Yanga inashika nafasi ya pili wakati wapinzani wao Polisi Tanzania wanashika nafasi ya sita.

Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha mpya wa Yanga Fadlu Davids ambaye alitua Jangwani mwanzoni mwa mwezi huu akichukua mikoba iliyoachwa na Manqoba Mngqithi.

Ni wazi utakuwa mchezo mgumu lakini kwa Yanga alama tatu ni matokeo muhimu zaidi ili kuendelea kuwa karibu na watani zao Simba kwenye mbio za ubingwa

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
14h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Happy Birthday GSM
Happy Birthday GSM
1d ago
READ MORE β†’