Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam wakitokea Moshi ambako jana waliibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Wananchi sasa wanahamisha nguvu zao kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ambapo Ijumaa ijayo Yanga itashuka uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kucheza mechi ya kwanza ya kundi B dhidi ya MC Alger.
Yanga inatarajiwa kuelea visiwani Zanzibar kukamilisha maandalizi yake.



