Yanayojiri Urusi : Uruguay yaifumua Urusi 3-0, yaongoza kundi A

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Uruguay yaifumua Urusi 3-0, yaongoza kundi A
Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Urusi wamekumbana na kipigo chao cha kwanza kwa kulazwa mabao 3-0 na Uruguay katika mchezo uliokuwa wa kumpata kinara wa kundi A kwa kuwa timu zote tayari zilikuwa zimefuzu hatua ya mtoano.

Mabao ya Luis Suarez, Denis Cheryshev (alijifunga) na Edison Cavan yameihakikishia Uruguay kumaliza kileleni mwa kundi A baada ya kufikisha alama tisa.

Uruguay sasa itachuana na mshindi wa pili wa kundi B katika hatua ya 16 bora wakati Urusi itamsubiri kinara wa kundi B.

Michezo ya kukamilisha mzunguuko wa tatu kundi B itapigwa leo Jumatatu, Juni 25 2018 saa tatu usiku ambapo Ureno itachuana na Irani wakati Hispania itacheza na Morocco michezo yote ikipigwa wakati mmoja.

Nayo Saudi Arabia imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kuilaza Misri mabao 2-1.

Mchezo huo ulikuwa wa kukamilisha ratiba tu kwa kuwa timu zote tayari zilikuwa zimeondoshwa mashindanoni.

Mohammed Salah aliitanguliza Misri kwa bao safi kwenye dakika ya 22 lakini Saudi Arabia ikasawazisha kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Salman Al Faraj.

Huo ulikuwa mkwaju wa penati wa pili kwa Saudia, mkwaju wa kwanza uliokolewa na mlinda lango mkongwe wa Misri El Haddary aliyeweka rekodi ya kucheza michuano hiyo akiwa na umri wa miaka 45.

Saudia ilifunga bao la ushindi kwenye dakika za majeruhi mfungaji akiwa Salem Al Dawsari
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’