Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31m ago
Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL

Pointi tisa za nyumbani na kuvuna nyingine ugenini ndiyo hesabu za Kocha Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, katika harakati za kukivusha kikosi hicho hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu huu.

Fadlu ameweka wazi kuwa hana mpango wa kucheza soka la kujihami, akiamini ubora na uzoefu wa wachezaji alionao unatosha kukabiliana na wapinzani wao katika Kundi B.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini anataka kuona Wananchi wakitumia silaha yao ya kushambulia kusaka matokeo, badala ya kuingia uwanjani wakiwa na hofu ya wapinzani.

“Kwa kikosi tulichonacho, hatuna sababu ya kupaki basi nyumbani. Tuna wachezaji wenye ubora na uzoefu wa kucheza mashindano haya. Tunapaswa kutumia ubora huo kutengeneza matokeo na kutafuta ushindi.”

POINTI TISA ZA NYUMBANI

Katika hesabu za Fadlu, kushinda michezo yote mitatu ya nyumbani kutaiweka Yanga katika mazingira mazuri ya kupigania tiketi ya robo fainali, hatua ambayo Wananchi wanatamani kuifikia baada ya kukwama kwenye makundi msimu uliopita.

Hata hivyo, kocha huyo hataki mafanikio ya kikosi chake kutegemea matokeo ya nyumbani pekee, akisisitiza umuhimu wa kupambana kusaka ushindi hata katika viwanja vya wapinzani.

“Mpango wetu ni kushinda michezo yote tunayocheza nyumbani. Tunajua umuhimu wa kupata pointi zote tukiwa mbele ya mashabiki wetu, lakini hilo halimaanishi tunakwenda ugenini kwa lengo la kujilinda pekee,” alisema

ANA DAWA YA MECHI ZA UGENINI

Kutokana na ugumu wa kucheza ugenini katika michuano ya Afrika, Fadlu amefichua kuwa benchi lake la ufundi lina mikakati maalumu kwa ajili ya michezo mitatu ambayo Yanga itacheza nje ya Tanzania.

Dhamira yake ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa na ushindani katika kila mchezo, huku wakitumia uwezo wa wachezaji wake kutengeneza nafasi na kuwapa wakati mgumu wapinzani.

“Tutakuwa na mpango maalumu kwa michezo yetu ya ugenini. Tunajua haitakuwa rahisi, lakini hatuwezi kwenda kucheza kwa lengo la kujilinda pekee. Tunataka kutafuta pointi hata tunapokuwa ugenini.”

Baada ya kuanza vyema majukumu yake kwa kuiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 20, sasa Fadlu anakabiliwa na mtihani wa kuthibitisha makali yake kwenye anga za kimataifa.

Jumamosi, Novemba 28, Wananchi watafungua pazia la hatua ya makundi kwa kuikaribisha MC Alger ya Algeria kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Baada ya mchezo huo, Yanga itasafiri kwenda Tunisia kuvaana na Club Africain Desemba 5, kabla ya kukutana na vigogo wa soka la Misri, Zamalek, Desemba 19 nchini Misri.

Yanga SC Stories

Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
26m ago
READ MORE β†’
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
18h ago
READ MORE β†’
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
19h ago
READ MORE β†’
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
19h ago
READ MORE β†’
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
1d ago
READ MORE β†’
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
1d ago
READ MORE β†’