Timu ya MC Alger inatarajiwa kuwasili nchini leo kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya Yanga.
Jumamosi, Novemba 28 Yanga itakuwa mwenyeji wa mabingwa hao wa Algeria katika mchezo wa kwanza kundi B utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Wakati MC Alger wakiwasili, mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wao tayari wako visiwani Zanzibar wakiendelea na maandalizi.
Yanga iliwasili Zanzibar mapema jana ambapo jioni kikosi kiliendelea na maandalizi chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Fadlu Davids.
Yanga imepata wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo hii ikiwa ni awamu ya pili ya maandalizi yao baada ya kambi ya siku 10 waliyofanya wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA.