Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi visiwani Zanzibar kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya MC Alger.
Baada ya kuwasili Zanzibar mapema jana, vijana wa kocha Fadlu Davids hawakuwa na muda wa kupoteza kwani jioni waliendelea kujiweka sawa kuelekea mtanange huo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Zanzibar, Fadlu alisema licha ya ugumu wa mchezo ulio mbele yao, mpango mkakati walioweka ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Fadlu amesema ili kuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua inayofuata, wanahitaji kutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kushinda kila mchezo na pia kuhakikisha wanapata alama kwenye mechi za ugenini.
Yanga imewasili Zanzibar ikiwa na morali kubwa, wachezaji wakionekana kupania kufanya vyema zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu baada ya kuishia hatua ya makundi kwa misimu miwili mfululizo.



