Kikosi cha Yanga leo kimefanya maandalizi ya mwisho uwanja wa New Amaan Complex kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya MC Alger.
Yanga pamoja na wageni wao MC Alger wote wamehitimisha maandalizi yao katika dimba hilo kwani siku ya kesho uwanja utatumika kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho (CAFCC).
Ijumaa saa 10 jioni Azam Fc itaikaribisha Al Ahly Tripoli katika mchezo wa CAFCC.
Yanga imepata wakati mzuri wa maandalizi visiwani Zanzibar wakipata siku tatu zaidi za maandalizi baada ya awali kuweka kambi ya siku 10 visiwani humo wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Kocha Fadlu Davids bado ana siku moja zaidi ya kuhitimisha maandalizi yake ya mwisho siku ya Ijumaa.

