Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema licha ya ubora wa wapinzani wao MC Alger, wamejipanga kuanza vyema kampeni ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL).
Yanga itaumana na MC Alger kesho Jumamosi katika mchezo wa kwanza kundi B utakaopigwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
"Utakuwa mchezo mgumu kwa sababu MC Alger ni timu nzuri lakini kwa wakati huu tumejipanga kuweza kuwakabili kwa sababu tunaanzia nyumbani"
"Jambo muhimu ni kuweza kupata alama tatu ili kujiwekea mazingira mazuri katika hatua hii ya makundi."
"Wachezaji wote tuko tayari na tunakwenda kupambana kupata alama tatu ili tuanze vyema."
"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani, tunahitaji mchango wao kwani wanaongeza hamasa uwepo wao utatuongezea ari na morali ya kupambana, "alisema Job
Kikosi cha Yanga kiliweka kambi ya siku chache visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo ambapo leo watahitimisha maandalizi yao tayari kushuka dimba la New Amaan Complex kuwania alama tatu.