Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14m ago
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL

MSHAMBULIAJI wa Al Ahli Tripoli ya Libya, Fiston Kalala Mayele, ameitabiria Yanga kufanya makubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu huu, akiamini Wananchi wana nafasi kubwa ya kufika mbali iwapo watajipanga vizuri.

Mayele, ambaye aliwahi kutamba na Yanga kabla ya kutimkia Pyramids FC ya Misri, ametoa kauli hiyo wakati kikosi cha Wananchi kikitarajiwa kushuka dimbani leo, Jumamosi, Novemba 28, kuanza safari ya kusaka tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo.

Yanga itawakaribisha MC Alger ya Algeria kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, katika mchezo wa kwanza wa Kundi B.

Akizungumza baada ya kuiongoza Al Ahli Tripoli kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) uliopigwa jana kwenye uwanja huo, Mayele amesema anaiona Yanga kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

AIPA YANGA NAFASI YA KUFIKA FAINALI

Kwa mtazamo wa Mayele, mbali na klabu yake ya zamani ya Pyramids FC, Yanga ni miongoni mwa timu zinazoweza kupigania nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo anaamini kutokuwepo kwa baadhi ya vigogo wa soka la Afrika, wakiwemo Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kunaongeza nafasi ya Wananchi kufanya makubwa.

“Ukiangalia Champions League msimu huu, ukimtoa Pyramid, kama kuna timu ambayo ile watu wanajua ya kwamba ndiyo timu inayoweza kufika fainali na Yanga ana nafasi kubwa. Wakijipanga vizuri wataenda mbali kwa sababu hakuna Al Ahly ya Misri, hakuna Mamelodi Sundowns,” amesema Mayele.

Kauli hiyo ya Mayele inaongeza hamasa kwa Wananchi ambao wana kiu ya kuona timu yao ikivuka hatua ya makundi baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa misimu miwili mfululizo.

MTIHANI WA KWANZA NI MC ALGER

Yanga ina kazi kubwa ya kuhakikisha inavuka katika Kundi B ambalo linazikutanisha timu za MC Alger, Club Africain ya Tunisia na Zamalek ya Misri.

Kocha Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, tayari ameweka wazi mikakati yake ya kushinda michezo yote ya nyumbani, huku akilenga pia kuvuna pointi katika michezo ya ugenini.

Mchezo wa leo dhidi ya MC Alger utakuwa kipimo cha kwanza cha uwezo wa kikosi hicho katika kutimiza malengo yake ya kimataifa.

Yanga SC Stories

Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
27m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
18h ago
READ MORE β†’
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
18h ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
20h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
1d ago
READ MORE β†’