Kazini kwa Mudathir kulikuwa na kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Kazini kwa Mudathir kulikuwa na kazi

Wanasema siku hazifanani, na kila mtafutaji ipo siku moja mbaya ambayo atakutana nayo ofisini. Ndivyo unavyoweza kuelezea kilichomkuta kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya, jana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya MC Alger.

Ni moja ya mechi ambazo Mudathir anapaswa kuzisahau haraka na kurejea kwa nguvu kwenye uwanja wa mazoezi, kwani kazi ndiyo kwanza inaanza.

Wakati Maxi Nzengeli akikosekana kutokana na majeraha, Kocha Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, alimkabidhi Mudathir jukumu kubwa la kuchezesha timu, lakini kwa bahati mbaya hakulifanya kwa ubora uliotarajiwa.

Mipira mingi ilipotea miguuni mwake, wakati mwingine alichelewa kufanya maamuzi, huku pasi zake nyingi zikielekezwa nyuma hata katika nyakati ambazo timu ilikuwa na nafasi nzuri ya kwenda kushambulia.

Mudathir alikosa ule utulivu, ubunifu na ujasiri wa kufanya maamuzi ambao tumezoea kuuona kutoka kwake anapokuwa katika kiwango chake bora.

Baada ya dakika 90 kumalizika, huku Yanga ikikubali kipigo cha bao 1-0, sura ya Mudathir ilieleza mengi. Alionekana wazi kutoridhishwa na kiwango alichokionyesha kwenye mchezo huo.

Hata hivyo, mchezo mmoja mbaya hauwezi kufuta ubora wa mchezaji. Kinachotakiwa sasa ni namna atakavyojibu baada ya kukutana na siku hiyo mbaya.

Itoshe kusema ilikuwa siku mbaya ofisini kwa Mudathir. Anapaswa kujitathmini, kurejea kwenye uwanja wa mazoezi, kusahihisha mapungufu yake na kurudi tena uwanjani akiwa bora zaidi.

Yanga ina takribani siku sita tu za kusahihisha makosa kabla ya kushuka tena dimbani katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Club Africain ugenini.

Yanga SC Stories

Hakuna kukata tamaa, kituo kinachofuata ni Club Africain
Hakuna kukata tamaa, kituo kinachofuata ni Club Africain
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 0-1 MC Alger, CAFCL MD1
FT : Yanga 0-1 MC Alger, CAFCL MD1
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs MC Alger, CAFCL, MD1
Kikosi : Yanga vs MC Alger, CAFCL, MD1
17h ago
READ MORE β†’
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
1d ago
READ MORE β†’
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
1d ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
1d ago
READ MORE β†’