Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten kwa mara nyingine amewataka wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga wenye shauku ya kufahamu usajili wa timu yao wawe watulivu kwa kuwa zoezi la usajili liko mbioni kukamilika.
Yanga imeanza mazoezi leo kwenye viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam ikiwa na wachezaji 14 wanaofanya majaribio.
Wachezaji kutoka Mataifa mbalimbali kama Nigeria, Congo DR, Congo Brazaville, Zambia, Kenya na kwingineko ni miongoni mwa wanaojaribiwa.
"Taarifa ya Kamati itatolewa baadae. Tusubiri kamati ya usajili ikamilishe kazi. Nadhani taarifa hiyo itatolewa siku si nyingi," amesema Ten.
"Wachezaji nane tuliokuwa nao msimu uliopita wamehudhuria mazoezi leo, na wengine 14 wamefika kufanya majaribio."
"Wachezaji wengine watawasili kesho kwa kufuata maelekezo ya program ya Mwalimu Zahera"

ADVERTISE HERE