Chirwa rasmi Ismailia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2018
Chirwa rasmi Ismailia
Sasa sio siri tena kwamba aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa msimu ujao atashiriki ligi kuu ya Misri akiitumikia klabu ya Ismailia.

Chirwa aliyekuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wake na Yanga aliondoka kimya kimya kwenda Misri kumalizana na Ismailia ambayo imefanikiwa kumsajili.

Mkataba wa Chirwa na Yanga umemalizika rasmi leo hivyo kumfanya awe mchezaji huru.

Chirwa ameitumikia Yanga kwa misimu miwili, akicheza takribani michezo 62 na kufunga mabao 32 katika michuano yote.



Kuondoka kwa Chirwa kulitarajiwa na wengi baada ya mkataba wake kumalizika kwani hakuwa miongoni mwa wachezaji 'wavumilivu' hasa wakati huu ambao Yanga imekumbwa na 'mdororo wa kiuchumi'.

Msimu uliopita, Chirwa mara kadhaa aliendesha migomo kushinikiza alipwe malimbikizo ya mishahara na fedha za usajili.



Licha ya udhaifu wake, Chirwa alikuwa mpambanaji, wakati mwingine alijitoa sana kuisaidia Yanga kupata matokeo.

Msimu uliomalizika aliibuka kinara wa upachikaji mabao kwenye ligi katika kikosi cha Yanga akifunga mabao 12.

Alifunga idadi kama hiyo ya mabao msimu wa 2016/17.

Kuondoka kwa Chirwa kunailazimu Yanga kusaka mbadala wake ambaye jina lake litatumwa CAF kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Donald Ngoma majina yao yalitumwa CAF kwa ajili ya michuano hiyo lakini sasa kwenye safu ya ushambuliaji amebaki Tambwe pekee baada ya Chirwa na Ngoma kuondoka.

Yanga ina nafasi tatu za usajili wa michuano ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’