Yanayojiri Urusi : Uingereza majaribuni dhidi ya Colombia leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Uingereza majaribuni dhidi ya Colombia leo
Uingereza inasaka nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la dunia huko Urusi leo itakapoikabili Colombia kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora utakaopigwa saa tatu usiku.

Kikosi cha Uingereza kilichosheheni wachezaji vijana kinaonekana kuimarika zaidi kwenye michuano ya mwaka huu.

Timu hiyo inayonolewa na kocha Gareth Southgate inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ingawa michuano hiyo imekuwa na 'maajabu'.

Uingereza haijawahi kufungwa na Colombia. Timu hizo zimekutana mara tano, Uingereza imeshinda mara tatu ya kutoka sare mara mbili.

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya kombe la dunia ilikuwa mwaka 1998 ambapo Uingereza iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Colombia ilianza michuano hiyo taratibu lakini imekuwa ikiimarika mchezo hadi mchezo.

Mwaka 2014 timu hiyo ilitinga robo fainali nchini Brazil na kuondoshwa na wenyeji. Kiungo James Rodriguez aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.

Uingereza itamtegemea zaidi kinara wake wa mabao Harry Kane ambaye ameifungia timu hiyo mabao matano akiwa ndiye anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.

Kabla ya mchezo huo, saa 11 jioni kutapigwa mchezo kati ya Uswisi dhidi ya Sweden.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Colombia na Uingereza kwenye hatua ya robo fainali.

Wengi wanaitabiria Uingereza itafanikiwa kutinga nusu fainali kama itaweza kuiondosha Colombia leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’