Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki uliokuwa na upinzani mkali kutoka kwa vijana wa Hans van Pluijm.
Singida United iliuanza mchezo huo kwa kasi na kupata penati mapema tu kwenye dakika ya kwanza baada ya nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro kumuangusha mshambuliaji wa Singida United, Usengimana.
Hata hivyo Singida United ilikosa penati hiyo baada ya mpigaji kupaisha langoni.

Kwenye dakika ya tano, Thabani Kamusoko aliiandikia Yanga bao la kuongoza kwa mpira murua wa adhabu baada Ibrahim Ajib kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.
Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Singida United iliyosawazisha kwenye dakika ya nane kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Usengimana.
Aidha Singida United iliendelea kutawala mchezo huo kwenye kipindi cha kwanza ikitumia udhaifu uliojitokeza kwenye safu ya ulinzi ya Yanga.
Pia sehemu ya kiungo haikuwa na maelewano mazuri kati ya Kamusoko, Buswita na Alpha jambo ambalo kwa hakika limechangiwa na 'upya' wa viungo Buswita na Alpha.
Wachezaji hao wamekuwa pamoja chini ya wiki hivyo tunatarajia muungano mzuri utapatikana tu.
Bao la pili la Singida United lilifungwa na Simbarashehe baada ya kuvunja mtego wa kuotea uliokuwa umewekwa na walinzi wa Yanga
Kwenye dakika ya 34, kocha Lwandamina alimtoa nahodha Nadir Haroub na kumuingiza beki Abdallah Shaibu 'Ninja' baada ya kugundua udhaifu kwenye ulinzi.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwa upande wa Yanga ambayo ilishindwa kutengeneza nafasi za mabao kutokana na vijana wa Singida United kukaba kwa pamoja na kufunga nafasi kwa haraka.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Hassan Kessy nafasi ya Juma Abdul, Emanuel Martin nafasi ya Ibrahim Ajib, Fernando Bongnyang nafasi ya Buswita, Tambwe nafasi ya Raphael Daudi.
Baadae Lwandamina alibadili kikosi chote kwa kuwatoa Kamusoko na Ngoma nafasi zao zikichukuliwa na Juma Mahadhi na vijana kutoka Yanga B Heri, Maka na Saidi Mussa ambao watatumika kwenye kikosi cha kwanza msimu huu.

Mabadiliko hayo yaliipa nguvu Yanga na kufanikiwa kusawazisha bao kwenye dakika ya 83 mfungaji akiwa Amissi Tambwe kupitia mkwaju wa penati.
Tambwe alifunga penati hiyo dakika mbili tu baada ya Atupele Green kukosa mkwaju wa penati langoni kwa Yanga, Youthe Rostand akizuia penati hiyo.
Yanga ilicharuka kwenye dakika za majeruhi na alikuwa ni Emanuel Martini aliyefunga bao la ushindi kwa shuti kali la nje ya 18.
Hadi mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mpambano huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Licha ya ushindi lazima tukiri kuwa mchezo huu ulikuwa mgumu sana kwa vijana wa Yanga. Lakini pia lazima tumpongeze Mwalimu Lwandamina kwani tunaanza kuona dalili njema kwenye kikosi cha Yanga.
Tumewashuhudia vijana wakizuia mashambulizi ya Singida United bila kuchoka, stamina ya wachezaji imeboreka.
Singida United ingeweza kufunga mabao mengi kama 'pumzi' ya vijana wa Yanga ingekata kutokana na mashambulizi mfululizo.
Pia nadhani kwa mchezo huu Mwalimu Lwandamina atakuwa amepata picha ni wachezaji gani awatumie kwenye kikosi chake cha kwanza.
Vijana walioingia kipindi cha pili walichangamsha mchezo zaidi.
Lazima tukiri pia kuwa muda wa kuendelea kumtegemea Nadir Haroub pale nyuma unazidi kuyoyoma, Abdallah Shaibu 'Ninja' amedhihirisha akichezeshwa michezo kadhaa mikubwa atakuwa mlinzi mahiri sana.
Bado kuna wiki tatu kabla ya mchezo wa ngao ya jamii, muda huo unatosha sana kwa Mwalimu Lwandamina kufanya mabadiliko kadiri anavyoweza ili kujenga Yanga imara zaidi.
Huu ulikuwa mchezo wa kirafiki tu, Yanga imeshinda lakini imepata alama sifuri, muhimu, utawasaidia walimu kuendelea kuboresha kikosi.
Lakini ushindi huu umeweza kuwanyamazisha wale wa upande ule ambao tunashukuru leo wametuchangia pesa ya kutosha kwa kujaa kwenye dimba la Taifa kuishangilia Singida United.
Nasikia timu yao ndio inarudi leo kwa mafungu kutoka huko walikoweka kambi lakini kwa jinsi Yanga ilivyo timu kubwa wameshindwa kwenda kuipokea timu yao na kuja uwanja wa Taifa kujumuika nasi ingawa mwisho wa siku wamerudi nyumbani vichwa chini!

ADVERTISE HERE