Mshambuliaji Heritier Makambo aliyekuwa akifanya majaribio katika timu ya Yanga amefuzu majaribio hayo na huenda akawa sehemu ya wachezaji wa timu hiyo wa msimu ujao.
Makambo aliyetokea klabu ya FC Lupopo ya DR Congo aliletwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera na kufanya majaribio sambamba na wachezaji wengine wapya.
Katika majaribio hayo Makambo alionyesha uwezo mkubwa na kumfanya awe miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kabisa waliopitishwa na benchi la ufundi la Yanga kwa ajili ya kusajiliwa.
Kuna taarifa kuwa jina la Makambo ni miongoni mwa majina matatu yaliyotumwa na Yanga CAF ili aweze kutumika kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika alithibitisha kuwa klabu hiyo tayari imetuma majina matatu ya wachezaji walioongezwa kwenye kikosi chake CAF.
Hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina ya wachezaji hao akieleza kuwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ndiye atakayezungumzia swala hilo.
Mbali na Makambo, wachezaji wengine wanaotajwa kuwa wamejumuishwa kwenye orodha hiyo ni winga Mrisho Ngassa na Deus Kaseke.

ADVERTISE HERE