Manji kurejea Yanga ni swala la muda tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2018
Manji kurejea Yanga ni swala la muda tu
Wanasema kimya kingi kina mshindo mkuu, hilo ndilo linalokwenda kutokea baada ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufu Manji kuwa mbioni kurejea kwenye nafasi yake.

Kumekuwa na ukimya tangu kupitishwa kwa Maamuzi ya Wanachama wa Yanga kumtaka Manji arejee kwenye nafasi yake baada ya kuikataa barua yake ya kujiuzulu.

Manji hakutoa kauli yoyote tangu alipoandikiwa barua na uongozi wa Yanga kumtaarifu uamuzi huo wa wanachama uliopitishwa kwenye Mkutano Mkuu Juni 10, 2018.

Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika alisema uongozi wa timu hiyo umeendelea kumsubiri Mwenyekiti wao huyo huku wakiamini alikuwa kimya sababu ametingwa lakini atarejea.

Habari njema ni kwamba Manji yuko mbioni kurejea na tayari ameiongezea nguvu za kifedha Kamati ya Tarimba ili kuweza kufanikisha masuala ya usajili.

Yanga ilipewa siku 60 na Serikali kuhakikisha imefanya uchaguzi kujaza nafasi zilizowazi. Uchaguzi huo bado haujaitishwa lakini huenda ukahusisha nafasi mbili za wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walijiuzulu.

Yanga pia inatarajiwa kuendeleza mchakato wa mabadiliko Manji atakapokuwa amerejea akiwa Mwenyekiti.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’