Makambo akabidhiwa jezi ya Ngoma Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2018
Makambo akabidhiwa jezi ya Ngoma Yanga
Mshambuliaji mpya wa Yanga Heritier Makambo atatumia jezi namba 11 iliyoachwa na Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC baada ya mkataba wake na Yanga kuvunjwa.

Makambo amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani mwezi sasa, amesajiliwa baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake.

Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu majaribio na vipimo vya afya.

Ni miongoni mwa wachezaji watatu walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Huenda akaanza kuonekana akiitumikia Yanga kwenye mchezo wa Jumatano ijayo dhidi ya Gor Mahia sambamba na Mrisho Ngassa na Deus Kaseke ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amethibitisha kutumwa kwa majina yao CAF.

Yanga inatarajiwa kuondoka keshokutwa kwenda nchini Kenya kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Julai 18 katika dimba la Moi jijini Nairobi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’