Mtu aliyefahamika kwa jina Christopher Paul jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook aliandika habari ya uzushi kuwa winga mpya wa Yanga Mrisho Ngassa amefariki dunia.
Mtu huyo anasakwa na jeshi la Polisi baada ya kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa hizo zilisababisha usumbufu kwa familia ya Ngassa, ndugu zake, rafiki zake pamoja na mashakibi wake walio ndani na nje ya nchi.
Ngassa ameeleza kusikitishwa na taarifa hizo ambazo ziliibua hofu kwa wazazi wake walio jijini Mwanza.
"Nimeumizwa sana na sijui kwanini huyu mtu kaandika lakini tumsamehe tu ila ajue tu amewashtua wazazi wangu na mimi pia mpaka sasa ninapoongea nipo na watu baadhi wamefika kutaka kujua ukweli kama nipo hai", amesema Ngassa.
Baadhi ya watu huenda hawajapata elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Kumzushia mtu kifo ni jambo baya, ni vyema mashabiki wa soka tukafahamu, soka ni burudani wala sio uadui.

ADVERTISE HERE