Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Mpito, Abbas Tarimba amefanikiwa kumzuia beki Kelvin Yondani asiweze kusajiliwa na Simba baada ya kufikia makubaliano ya kuhuisha mkataba wake.
Jana Yondani alifanya mazungumzo na Tarimba, mazungumzo ambayo yamezima jaribio la klabu ya Simba kutaka kumsajili baada ya kukubali kusaini mkataba mpya.
Licha ya uongozi wa Simba kupitia msemaji wao Haji Manara kukanusha kuwa hawakuwa na mpango wa kumsajili Yondani, ukweli ni kwamba juzi viongozi wa Simba walifanya mazungumzo na Yondani.
Wametoa tamko hilo baada ya jaribio lao la kutaka kumsajili beki huyo kisiki kushindwa.
Tarimba ambaye bado amesisitiza kujiondoa katika uongozi wa Kamati Maalum ya mpito, pia amefanikisha kumbakisha kikosini beki Hassani Kessy.
Tarimba amesema licha ya kujiondoa kwenye uongozi, yeye bado ni mwanachama wa Yanga hivyo haoni tatizo kuisaidia timu yake katika masuala mbalimbali.

ADVERTISE HERE