Viongozi Yanga chukueni maamuzi magumu

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
21 Jul 2018
Viongozi Yanga chukueni maamuzi magumu
Kwa hali inayopita Yanga wakati huu ingefaa Makamu Mwenyekiti Clement Sanga akaitisha Mkutano Mkuu kwa ajili ya kujaza nafasi zilizowazi ikiwemo ya Mwenyekiti, Yusuph Manji.

Muda wa miezi mitatu aliotoa mfanyabiashara huyo ni mrefu sana. Yanga inahitaji kusimama wakati huu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom August 22, 2018.

Baada ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu Charles Mkwasa, idadi ya viongozi ambao wameachia ngazi Yanga imefikia sita.

Idadi hiyo ni kubwa sana, ilipaswa viongozi wa Yanga waliopo wachukue hatua za haraka kujaza nafasi hizo.

Serikali iliipa Yanga siku 60 kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi.

Zimebaki takribani siku 20, naamini amri hii ya Serikali haikwepeki. Tuna imani Sanga ataitisha Mkutano Mkuu wa dharura.

Pia zipo taarifa kuwa tangu Mkwasa ajiuzulu, Yanga haina mtendaji Mkuu kwa kuwa nafasi yake bado haijakaimiwa.

Hali hiyo inawapa hofu wadau wa Yanga hasa wakati huu ambao anahitajika kiongozi wa kusimamia shughuli za klabu za kila siku.

Inadaiwa kuchelewa kutumwa kwa majina ya Ngassa, Kaseke na Makambo CAF kumechangiwa na uzembe uliofanyika baada ya kukosekana msimamizi wa mchakato huo.

Kwa sasa Yanga inamtegemea zaidi Afisa Habari wake Dismas Ten kusimamia michakato hiyo ingawa hayo sio majukumu yake ya msingi.

Baada ya Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi ni vyema mchakato wa mabadiliko ukakamilishwa kwa haraka. Kinachoitesa Yanga wakati huu ni mfumo wa kutegemea mfuko wa mtu mmoja.

Wakati huu Yanga inakwama kufanya mambo yake kwa kuwa viongozi wamebweteka baada ya Manji kuahidi anarejea katika kipindi cha miezi mitatu.

Na hata Manji akirejea, naamini Yanga haipaswi kuendelea kuutegemea mfuko wake pekee bila ya kuwa na mfumo unaojiendesha bila ya uwepo wake.

Kwani kama alipata matatizo yaliyomfanya ajiweke pembeni, itakuwaje siku akipata matatizo mengine? Yanga itaendelea na mfumo huu mpaka lini?

Njia sahihi ni kwa viongozi kukubali mchakato wa mabadiliko ukamilishwe, timu iwe kampuni, iuze hisa na ikabidhiwe kwa wawekezaji ambao wataiendesha kitaalamu.

Ni jambo la aibu kwa Yanga pale wachezaji wake wanapogoma kushinikiza walipwe stahiki zao. Wakati mwingine sisi mashabiki tunakosea tunapowalaumu.

Mpira ndio kazi yao. Wana familia ambazo zinawategemea kwa mahitaji ya kila siku. Sasa wanapokosa mishahara wafanyeje?

Makosa ni ya viongozi wa timu yetu kwa kusuasua kuchukua maamuzi yatakayoiwezesha Yanga kujitegemea na kuondokana na haya yanayotokea.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’