Ninja awatuliza mashabiki Yanga

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
8 Aug 2017
Ninja awatuliza mashabiki Yanga
Beki mpya wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia, kikosi cha Yanga kiko imara tayari kupambana na mpinzani yeyote.

Shaibu aliyesajiliwa na Yanga kutoka Taifa ya Jan'gombe ni mmoja wa maingizo mapya msimu huu.

Shaibu amesajiliwa baada ya klabu ya Yanga kuachana na mlinzi raia wa Togo Vicent Bossou.

"Kikosi chetu kiko vizuri, ukiangalia mpaka sasa tupo vizuri katika kila idara na tupo tayari kupambana na timu yoyote ile ambayo itakuja mbele yetu, kwa kifupi tumejiandaa vema kuanza ligi," amesema

"Najua kila timu imejipanga vizuri kuhakikisha inafanya vizuri msimu ujao, lakini niwaambie tu, sisi tupo vizuri zaidi, hivyo wajiandae na vichapo."

Tayari uwezo wa mlinzi huyo umeanza kuwa gumzo na anatabiriwa kuwa mmoja wa walinzi hodari kabisa.

Aliichezea Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United ambapo aliingia kwenye dakika ya 34 kuchukua nfasi ya nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’