Sapoti ya mashabiki inahitajika uwanja wa Taifa kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2018
Sapoti ya mashabiki inahitajika uwanja wa Taifa kesho
Kesho Jumapili, Julai 29 2018 Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Gor Mahia kwenye mchezo wa duru ya pili michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa kikosi cha Yanga kwani kama itaibuka na ushindi itarejesha matumaini ya kutinga robo fainali kama itafanya vizuri kwenye michezo mingine miwili itakayokuwa imebaki.

Kinachoibeba Yanga dhidi ya wapinzani wake Gor Mahia na Rayon Sports ni kuwa na michezo miwili nyumbani.

Sasa ikiwa na alama moja, ikiibuka na ushindi kwenye michezo hiyo dhidi ya Gor Mahia na USM Alger itafikisha alama saba kabla ya kwenda kuikabili Rayon Sports ugenini.

Gor Mahia ina mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya Rayon wakati Wanyarwanda hao watabakisha mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya Yanga.

Gor Mahia na Rayon zote zitakwenda Algeria kuivaa USM Alger. Hakutakuwa na urahisi kwa timu hizo kuibuka na ushindi Algeria.

Baada ya kukamilika kwa michakato ya usajili, wachezaji wa Yanga sasa wamehamishia akili zao kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Kufungwa mabao 4-0 na Gor Mahia kwenye mchezo uliopita kwa kiasi kikubwa kulichangiwa na wachezaji kutokuwa mchezoni kutokana na changamoto zilizokuwa zinawakabili.

Kulikuwa na wachezaji ambao hawakuwa na mikataba huku ikielezwa wengine walikuwa wakidai mishahara yao. Lakini changamoto hizo zimetatuliwa na uongozi wa Yanga.

Yanga imekuwa ikijifua kikamilifu kujiandaa na mchezo huo huku Kocha Mwinyi Zahera akiahidi kuja na mbinu tofauti na mchezo uliopita.

Sapoti kubwa ya mashabiki inahitajika uwanjani ili kuwapa nguvu wachezaji.

Viingilio vya mchezo hio 'vimepozwa' ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kuushuhudia mchez huo utakaoanza saa moja jioni.

Kwa Jukwaa la VIP A kiingilio ni Tsh 10,000/- wakati VIP B na C ni Tsh 7,000/- huku upande wa mzunguuko ikiwa Tsh 3,000/-
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’