Yanga imepania kupindua meza kibabe leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2018
Yanga imepania kupindua meza kibabe leo
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Gor Mahia katika mchezo utakaopigwa saa moja kamili jioni.

Huo ni mchezo wa mzunguuko wa nne wa kundi D.

Timu hizo zilikutana Julai 18 katika mchezo wa mzunguuko wa tatu uliopigwa jijini Nairobi na Yanga kulazwa mabao 4-0.

Mchezo wa leo una umuhimu wa kipekee kwa Yanga kwani ni lazima ishinde ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Naye Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuongeza nguvu ya kikosi cha Yanga.

Viingilio vya mchezo huo vimerahisishwa ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kufika uwanjani.

Jukwaa la VIP A tiketi zinapatikana kwa Tsh 10,000 wakati VIP B na C ni Tsh 7,000/- na upande wa mzunguuko ikiwa Tsh 3,000/- tu.

Katika msimamo wa kundi D USM Alger inaongoza ikiwa na alama saba ikifuatiwa na Gor Mahia yenye alama tano.

Rayon Sports inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili wakati Yanga inashika nafasi ya nne ikiwa na alama moja.

Yanga ndio timu pekee ambayo haijafunga bao kwenye michuano hiyo huku ikiwa imeruhusu mabao nane kutikisa nyavu zake.

Yanga imeimarika zaidi baada ya kurejea kwa Kelvin Yondani kwenye safu ya ulinzi huku Deus Kaseke na Matheo Anthony wakitarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Naye kiungo Thabani Kamusoko ambaye alikosa mchezo uliopita huenda akarejea kikosini kwenye mchezo wa leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’