Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka juu ya mipango ya klabu hiyo kuanza kuuza jezi na vifaa vyake vingine ili kujiingizia mapato.
Mfumo huo utaiwezesha Yanga kuingia mkataba na kampuni ambayo itakubaliana nayo kwaajili ya kusambaza vifaa kama jezi, skafu, vikombe vyenye nembo ya klabu vingine vingi kwa nchi nzima.
Akizungumzia mipango hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Omary Kaaya alisema klabu hiyo endapo itapata kampuni ambayo wataingia nayo makubaliano watakuwa na mambo mengi ya kufanya kupitia nembo ya timu hiyo.
"Biashara ya klabu siyo jezi peke yake, unaweza ukauza peni, skafu, vikombe na vingine, lakini lazima kuwe na utaratibu rasmi wa kufanya hivyo vitu, kwenye taasisi kama hii kuna taratibu zake na tunaangalia pia kampuni sahihi ya kufanya nayo kazi bila kuwa na mianya yoyote ya kudhulumiana," alisema.
βNi kitu ambacho kipo, kitakuja na hakikwepeki na sio kwa jezi tuu, ni kwenye vitu vyote ambavyo vitainufaisha klabu β. Aliongeza Kaaya.
Katika hatua nyingine Kaaya alito onyo kwa watu wanaochapisha na kuuza jezi za klabu hiyo kuwa wakati rasmi wa klabu kuuza vifaa vyao wenyewe ukifika watachukuliwa hatua za kisheria ili kupunguza tatizo hilo na hatimaye klabu iweze kupata faida.
Klabu ya yanga kwa sasa iko katika maandalizi Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu Tanzania bara.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE