Yanga yasaka kampuni ya kuuza bidhaa zake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2018
Yanga yasaka kampuni ya kuuza bidhaa zake
Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka juu ya mipango ya klabu hiyo kuanza kuuza jezi na vifaa vyake vingine ili kujiingizia mapato.

Mfumo huo utaiwezesha Yanga kuingia mkataba na kampuni ambayo itakubaliana nayo kwaajili ya kusambaza vifaa kama jezi, skafu, vikombe vyenye nembo ya klabu vingine vingi kwa nchi nzima.

Akizungumzia mipango hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Omary Kaaya alisema klabu hiyo endapo itapata kampuni ambayo wataingia nayo makubaliano watakuwa na mambo mengi ya kufanya kupitia nembo ya timu hiyo.

"Biashara ya klabu siyo jezi peke yake, unaweza ukauza peni, skafu, vikombe na vingine, lakini lazima kuwe na utaratibu rasmi wa kufanya hivyo vitu, kwenye taasisi kama hii kuna taratibu zake na tunaangalia pia kampuni sahihi ya kufanya nayo kazi bila kuwa na mianya yoyote ya kudhulumiana," alisema.

β€œNi kitu ambacho kipo, kitakuja na hakikwepeki na sio kwa jezi tuu, ni kwenye vitu vyote ambavyo vitainufaisha klabu β€œ. Aliongeza Kaaya.

Katika hatua nyingine Kaaya alito onyo kwa watu wanaochapisha na kuuza jezi za klabu hiyo kuwa wakati rasmi wa klabu kuuza vifaa vyao wenyewe ukifika watachukuliwa hatua za kisheria ili kupunguza tatizo hilo na hatimaye klabu iweze kupata faida.

Klabu ya yanga kwa sasa iko katika maandalizi Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu Tanzania bara.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’