Yanga yataja sababu ya Ajib, Tshishimbi kutokuwa kambini Morogoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2018
Yanga yataja sababu ya Ajib, Tshishimbi kutokuwa kambini Morogoro
Yanga imewasili mkoani Morogoro jana kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho.

Baadhi ya wachezaji hawakusafiri na timu kutokana na sababu mbalimbali.

Mapema leo Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten aliwaambia waandishi wa habari kuwa wachezaji wengine wanatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro kuanzia kesho.

Ibrahim Ajib, Ramadhani Kabwili na Papi Tashishimbi ni miongoni mwa wachezaji ambao bado hawajatua mkoani Morogoro.

Wakati Ajib akiwa na ruhusa kushughulikia tukio la kuvamiwa biashara yake, Tshishimbi na Kabwili wao walikuwa na masuala ya kiofisi ambayo Ten amesema tayari yamemalizika na watakwenda mkoani Morogoro wakati wowote.

Wakati huo huo Yanga imetangaza rasmi kuachana na mlinda lango Youthe Rostand baada ya yeye mwenyewe kuomba aachwe kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Rostand atalipwa fedha zake zote baada ya mkataba wake kuvunjwa.

Yanga ilikuwa na mpango wa kumtoa Rostand kwa mkopo hata hivyo mwenyewe ameona hayuko sawa kisaikolojia hivyo kuomba aachwe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’