Yanga kujipima dhidi ya Mkamba Rangers Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2018
Yanga kujipima dhidi ya Mkamba Rangers Jumatano
Timu ya daraja la pili ya Mkamba Rangers ya Kilombero, kesho Jumatano inacheza mechi ya kirafiki na Yanga, mchezo ambao umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa CCM, Mkamba Kilosa mkoani Morogoro.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili, huku Yanga ikiajiandaa na mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya USM Alger ya Algeria ambao umaengwa kufanyika Agosti 19 kwenye uwanja wa Taifa jijini.

Mmoja wa viongozi wa Mkamba Rangers, Juma Ligonela alisema kuwa waliongea na uongozi wa klabu ya Yanga kuhusiana na mchezo huo na kukubaliana.

Alisema kuwa mchezo huo pia utakuwa fursa kwa timu yao kuwapima wachezaji wapya na kuwaona wachezaji nyota wa yanga ambao wamejiunga msimu huu.

β€œTumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo na utakuwa wa pili kucheza na timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Mara ya kwanza walicheza na timu Mbeya City ya Mbeya na baadhi ya timu nyingine na kupata matokeo mazuri,” alisema Ligonela.

Kocha wa Mkamba Rangers, Juma Omary Mpoka alisema kuwa watatumia fursa hiyo kukitambulisha kikosi chao na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa msimu huu.

Mpoka alisema kuwa wamesajili wachezaji wengi chipukizi na wenye vipaji hivyo Yanga itegemee kupata upinzani mkali.

β€œPia tumesajili wachezaji wakongwe, tuna Semmy Kessy na wengine ambao wataonekana wakaonekana kwa mara ya kwanza kwenye mechi hiyo,” alisema Mpoka.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’