Yanga 'kuliamsha dude' uwanja wa Taifa leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2018
Yanga 'kuliamsha dude' uwanja wa Taifa leo
Mabingwa wa kihistoria wa soka Tanzania, Yanga leo wanashuka uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2018/19 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga inaanza kampeni ya kutwaa ubingwa iliyoupoteza msimu uliopita kwa watani zao wa jadi Simba kwa kuwakabili mabingwa wa kombe la FA Mtibwa Sugar katika mchezo unaotarajiwa kuanza saa 12 kamili jioni.

Kuelekea mchezo huo Yanga itawakosa wachezaji wawili, Juma Mahadhi na Mohammed Issa 'Banka' ambao ni majeruhi.

Vijana wa Jangwani wanaonolewa na Mcongoman Mwinyi Zahera wana shauku kubwa ya kuanza msimu kwa kishindo kikuu.

Yanga imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria.

Ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Yanga dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho umeongeza ari na kujiamini kwa wachezaji lakini pia umerejesha imani ya mashabiki kwa timu yao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’