Yanga ikiitumia vyema ratiba hii, Septemba 30 ni kicheko tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2018
Yanga ikiitumia vyema ratiba hii, Septemba 30 ni kicheko tu
Baada ya mapumziko ya wiki mbili za kalenda ya FIFA, ligi kuu ya Tanzania Bara itaendelea Septemba 15 ambapo Septemba 16 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United.

Yanga itakuwa na michezo mitatu mfululizo jijini Dar es salaam kwani baada ya mchezo dhidi ya Stand United, Septemba 19 itacheza na Coastal Union kabla ya kuivaa Singida United Septemba 23.

Kama ratiba hiyo itabaki ilivyo, ushindi katika michezo hiyo mitatu utaiweka Yanga katika mazingira mazuri kabla ya mchezo dhidi ya Simba ambao utafuata baada ya kumenyana na JKT Tanzania.

Hali ni tofauti kwa Simba ambayo itakabiliwa na michezo mitatu mfululizo ya ugenini dhidi ya Ndanda, Mbao FC na Mwadui) kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kucheza na Biashara kisha kufuata mchezo dhidi ya Yanga.

TFF iliipangia Simba michezo mitatu mfululizo jijini Dar es salaam mwanzoni mwa msimu huku Yanga ikipangiwa ratiba kama hiyo mikoani.

Hata hivyo kukosekana kwa uwanja mkoani Morogoro kuliinusuru Yanga kuanza na ratiba hiyo baada ya TFF kulazimika kuhamisha mchezo dhidi ya Mtibwa jijini Dar es salaam baada ya Chama cha Mapinduzi mkoani Morogoro kuzuia uwanja wake kwa ajili ya matumizi mengine.

Mchezo uliokuwa unafuata dhidi ya Kagera Sugar uliokuwa upigwe mkoani Kagera nao ukaahirishwa kutokana na Yanga kukabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports.

Jana tena TFF imeahirisha mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya Yanga na ule wa Simba dhidi ya Lipuli na Azam FC dhidi ya African Lyon baada ya kocha Mkuu wa timu ya Taifa Emanuel Ammunike kuwataka kambini mapema wachezaji wa Stars wanaochezea vilabu hivyo.

Matukio hayo yameifanya Yanga ianze na ratiba 'rafiki' zaidi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’