Zawadi ya mshindi TPL bado haifahamiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2018
Zawadi ya mshindi TPL bado haifahamiki
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekiri kwamba hadi sasa haijulikani bingwa wa ligi kuu Tanzania bara atapata zawadi gani baada ya aliyekuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kujiweka pembeni hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema, pamoja na hayo TFF bado ipo kwenye mazungumzo na makampuni mbalimbali nchini kuhakikisha kwamba bingwa anapata zawadi inayostahili kulingana na ligi husika.

"Baada ya kusema ligi inaanza bila udhamini, mdhamini amejiondoa kuna vitu vingi bado vinafanyiwa kazi na Vodacom kabla ya taarifa rasmi kutoka kama wataendelea au hawatoendelea lakinini bado tupo kwenye majadiliano makubwa," amesema Kidao

"Bado tubajadiliana na makampuni mengi kwa ajili ya kupata co-sponsors wengi ambao ukiwaunganisha wanaweza kutengeneza thamani kubwa ya ligi. Ni vitu ambavyo vinafanyika kwa nguvu kubwa.

"Vingozi wa taasisi na mimi hatulali tunafanya kazi kubwa kubwa kuhakikisha mzunguko wa ligi wa raundi ya 6, 7 au 8 tunapata mdhamini mkuu lakini kupata co-sponsors ni kitu kikubwa zaidi kwa sababu tutapata watu wadogowadogo lakini wengi ligi itakuwa na thamani kubwa.

"Ni vyema tuipe thamani ligi yetu inawezekana tunapita kipindi kigumu lakini mwisho wa siku thamani ya ligi itaonekana.

"Kuhusu bingwa atapewa nini mshindi wa pili na watatu na zawadi nyingine ni kitu tofauti, tutakapokuwa tumepata mdhamini mkuu na wadhamini wenza tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua bingwa atapata kitu gani kwa sababu kati ya proposal tulizokuwa tunapeleka zimekuwa zinaonesha kiwango ambacho bingwa anapaswa kupata kwa maana ya kuongoza kiasi ambacho anapaswa kupata bingwa.

"Hatuwezi kusema bingwa atapata nini hadi pale tutakapokuwa tumekubaliana na mdhamini juu ya yale tuliyoyaainisha kama sehemu ya udhamini wa ligi kuu.

"Inawezekana mazungumzo yakashindikana kwa mdhamini mmoja lakini bado haimaanishi ligi itachezwa bila mdhamini mpaka mwisho.

"Tumekuwa tukifanyia kazi hili jambo kwa kiwango kikubwa, tuna watu wengi ambao tunafanya nao mazungumzo. Tunaendelea kulinda thamani ya ligi yetu kwa kiwango ambacho ligi yetu inapaswa kuwa inadhaminiwa"

Kwa hisani ya Shaffih Dauda
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’