Beki Mtibwa Sugar akiri Makambo ni habari nyingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Sep 2018
Beki Mtibwa Sugar akiri Makambo ni habari nyingine
Mlinzi aliyefanikiwa kuwakaba washambuliaji Heritier Makambo wa Yanga na Meddie Kagere wa Simba, Kassian Ponela wa Mtibwa Sugar, amesema baada ya kuwavaa nyota hao anaona Makambo ni bora zaidi.

Washambuliaji hao kwa sasa ni gumzo kutokana na kuanza ligi kwa kasi kubwa, Kagere ndiye kinara wa mabao Simba akiwa nayo matatu aliyofunga kwenye mechi mbili na Makambo amefunga bao moja tu.

Ponela amesema kuwa Makambo ambaye alifanikiwa kucheza naye kwenye mechi ya ligi kuu msimu huu, ana nguvu na anajua kupambana na mabeki ukilinganisha na Kagere pamoja na Emmanuel Okwi wanaocheza Simba.

Beki huyo wa kati aliongeza kuwa alipata shida sana kumkaba Makambo alipokutana naye na alijitahidi kumzuia asifunge lakini alishindwa kutokana na uwezo mkubwa alionao mchezaji huyo.

β€œKwangu mimi namuona Makambo kuwa ni bora zaidi, nasema hivyo kwa sababu ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho mshambuliaji, ana nguvu, kasi, uwezo wa kumiliki mpira, anajua kupiga chenga lakini pia siyo muoga wa kupambana na mabeki wakorofi.

β€œOkwi yeye ni mzuri, ana kasi na anajua kumiliki mpira lakini hana nguvu pia ni muoga wakati Kagere yeye siyo muoga, ana nguvu, kasi na uwezo wa kupambana lakini siyo mzuri sana katika kumiliki mpira na kupiga chenga, kwa hiyo Makambo yupo vizuri,” alisema Ponela.

Championi
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’