Wagabon kuzichezesha Uganda vs Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2018
Wagabon kuzichezesha Uganda vs Stars
Waamuzi kutoka nchini Gabon, Eric Arnaud Otogo Castane, Montel na Issa Yaya watachezesha mchezo wa Jumamosi kati ya Uganda dhidi ya Tanzania.

Mchezo huo utakaopigwa keshokutwa, Septemba 08 dimba la Mandela jijini Kampala ni wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019.

Mwamuzi wa kati katika pambano hilo atakuwa, Eric Arnaud
Otogo Castane akisaidiwa na Mwamuzi Moussounda Montel
na Issa Yaya.

Stars inatarajiwa kuondoka leo mchana kuelekea nchini Uganda ikiwa na kikosi chake kamili tayari kwa mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amewataka Watanzania wote kuiunga mkono timu yao.

Amunike amesema timu hiyo ikifanya vizuri ni fahari kwa kila Mtanzania na isipofanya vizuri ni fedheha kwa kila Mtanzania pia.

Amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kuikabili Uganda na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’