TAKUKURU yapitia mikataba ya wachezaji Yanga

Habari247 By Habari247
β€’
6 Sep 2018
TAKUKURU yapitia mikataba ya wachezaji Yanga
Majina matatu ya wachezaji wa Yanga yametua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), huku mikataba yao nayo ikiwasilishwa katika taasisi hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilizothibitishwa na kiongozi mmoja, ambaye hakupenda kutajwa jina lake, zinasema Takukuru mara baada ya kutua Yanga wameomba mikataba ya wachezaji watatu wa timu kwa uchunguzi zaidi.

Mikataba ambayo imeombwa na Takukuru ni wa winga kinda, Burhan Akilimali β€˜Kiberenge’ aliyesajiliwa msimu uliopita. Mbali na Akilimali pia Yanga imepeleka taarifa ya usajili wa beki Mkongomani, Fistoo Kayembe, ambaye alikaribia kabisa kutua Yanga.

Kayembe alisajiliwa na Yanga, lakini klabu yake ya Sangabalenge ikagoma kumwachia ikidai bado ana mkataba, hivyo kuzuia hati yake ya uhamisho (ITC).

Pia, klabu hiyo ilitaka ilipwe Dola 5000 (Sh11 milioni) kama ada ya uhamisho, lakini Yanga iligoma na kukubaliana kumsubiri amalize mkataba.

Mbali na hao pia mkataba wa kiungo kiraka, Jafary Mohamed aliyesajiliwa msimu huu akitokea Majimaji ya Songea nao umepelekwa Takukuru. Hata hivyo, inaelezwa kuwa baadhi ya vigogo wa Yanga nao wanaweza wakaitwa kujieleza juu ya mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya klabu hiyo.

Kutokana na taarifa hiyo, Mwanapoti lilimtafuta Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye hakukubali wala kukataa juu ya suala hilo, lakini akasema hayuko kwenye wakati sahihi kulizungumzia.

β€œKwa sasa siwezi kusema hilo lipo au halipo, hatuoni kama kuna sababu ya kulitolea ufafanuzi kwa wakati huu, kama tutakuwa na kitu cha kuwaeleza tutafanya hivyo wakati ukifika,” alisema Misalaba

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’