Stars kuanza kuiwinda Cape Verde mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2018
Stars kuanza kuiwinda Cape Verde mapema
Taifa Stars itacheza na Cape Verde Oktoba 10, mwaka huu ugenini kabla ya kurudiana nchini siku tatu baadaye.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini juzi, Kocha Msaidizi wa Stars, Hemed Moroco, alisema wanatarajia kuingia kambini mapema (Septemba 24) kujiwinda kwa ajili ya mchezo huo.

Morocco alisema kambi hiyo inatarajiwa kuwa ya wiki mbili na kikubwa itakuwa kwa ajili ya kufanyia marekebisho baadhi ya mapungufu waliyoyaona kwenye mchezo dhidi ya Uganda.

"Tunataka kuongeza kitu kwenye kikosi chetu, kambi ya mapema ni suala muhimu kwa sababu tutacheza mchezo unaofuata 'away' (ugenini)," alisema Morocco.

Morocco alisema wanaocheza soka nje ya nchi wanaweza wakachelewa kuungana nao, lakini kwa wale wa ndani wataanza nao maandalizi mapema.

Stars ina pointi mbili baada ya kucheza michezo miwili na yote kutoka sare, imezidiwa kwa pointi mbili na Uganda wanaoongoza Kundi lao la L, huku Lesotho ambao walitoka nao sare kwenye mchezo wa kwanza wakilingana nao pointi, Cape Verde inaburuza mkia kwa kuwa na pointi moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’