Meneja wa Yanga Nadir Haroub amesema timu hiyo ilipunguza kasi baada ya kufunga mabao manne na kuwapa nafasi Stand United kuweza kumiliki mpira.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili jioni.
Mpaka dakika ya 57 Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 4-1. Hata hivyo baada ya kuingia mabao hayo Stand United ilikuja juu na kufanikiwa kurejesha mabao mawili.
"Baada ya kufunga mabao manne tulipoteza umakini na kuwaruhusu Stand United waweze kumiliki mpira," amesema Nadir baada ya mchezo.
"Tulikuwa na nafasi ya kuondoka na ushindi mnono zaidi lakini Stand United waliweza kutumia udhaifu wetu na kufanikiwa kufunga mabao mawili"
"Tutayafanyia kazi mapungufu haya yaliyojitokeza leo. Muhimu tunawataka mashabiki wa Yanga waendelee kutuunga mkono."
Jumatano Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Coastal Union katika mwendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara, mzunguuko wa tano.

ADVERTISE HERE