Tulijua tutateseka mwishoni - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2018
Tulijua tutateseka mwishoni - Zahera
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa Jumatano usiku.

Akizungumzia tatizo la wachezaji kuchoka hasa kwenye kipindi cha pili, Zahera amesema alifahamu hilo litatokea kutokana na wachezaji kutopata mapumziko ya kutosha baada ya mchezo uliopita.

"Tulicheza tarehe 16, tumepumzika siku mbili ya tatu tuko uwanjani. Mazoezi tumefanya siku mbili hivyo tulifahamu kuna wakati kwenye kipindi cha pili tutateseka sana," amesema Zahera baada ya mchezo huo.

"Mpango wetu ilikuwa kucheza kwa kasi kwenye kipindi cha kwanza kuhakikisha tunafunga mabao mengi ili kipindi cha pili tucheze kwa tahadhari"

Hata hivyo Zahera amekosoa matukio yanayofanywa na wachezaji wake na kupelekea wasipate ushindi mnono zaidi.

"Wachezaji wangu wana tatizo moja, wakishafunga wanapoteza umakini.

"Angalia mchezo dhidi ya USM Alger tulikuwa tunashinda 2-0, hivyo hivyo dhidi ya Mtibwa Sugar tulikuwa 2-0 mbele, dhidi ya Stand United tulikuwa tunashinda 4-1.

"Leo tulikuwa na uwezo wa kufunga mabao mengine mawili kupitia mashambulizi ya kushitukiza, lakini wachezaji walifanya uzembe."

Zahera amemwagia sifa kiungo Ibrahim Ajib kuwa sasa ameanza kubadilika kwani amekuwa akijituma uwanjani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’