Bossou bado hajapewa mkataba mpya

Admin By Admin
β€’
19 Jun 2017
Bossou bado hajapewa mkataba mpya
Beki kisiki raia wa Togo Vicent Bossou ambaye yuko mapumziko nchini kwao bado hajapewa mkataba mpya na uongozi wa Yanga, imefahamika.

Bossou aneyewaniwa na Singida United amesema kuwa atarejea nchini hivi karibuni ili kuja kusikiliza kama ataongezewa mkataba au la.

Licha ya kuisaidia Yanga msimu uliopita, Bossou ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakigoma mara kwa mara wakidai mishahara yao.

Katika mchezo wa VPL ambao Yanga ilichapwa mabao 2-1 na Simba, Bossou aligoma kucheza na alitoweka kambini siku moja kabla ya mchezo kushinikiza alipwe malimbikizo ya mishahara yake.

Mara kadhaa alirushiana maneno na mashabiki wa Yanga kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tabia yake ya kugoma kucheza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’