Rekodi za michezo ya Ngao ya Jamii

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
17 Aug 2017
Rekodi za michezo ya Ngao ya Jamii
Agosti 23, 2017 nyasi za Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam zitawaka moto kwa wapinzani wa jadi Tanzania Simba na Yanga kucheza katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Mchezo wa Ngao ya Jamii huwa ni sehemu ya ufunguaji wa pazi wa Ligi kwa msimu upya, ambapo kwa Tanzania kiasi cha pesa zinazopatikana kutokana na kingilio hutolewa kwa wa jamii ya watu wenye matatizo ya kiafya, matibabu na maisha duni.

Tangu kuanzishwa kwa Ngao ya Jamii mwaka 2001, klabu ya Yanga inaongoza kwa kutwaa Ngao hiyo ikiwa imeitwaa mara 5 ikifuatiwa na Simba iliyotwaa mara 4, na kufanya mchezo ujao kuwa mgumu kwa kila timu kutaka kufanya vizuri.

Yafuatayo ni matokeo ya michezo ya Ngao ya Jamii tangu ilipoanzishwa.

1. Yanga 2-1 Simba (2001)Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yusuph Tigana huku la Simba likifungwa na Steven Mapunda 'Garincha'

2. Mtibwa 1-0 Yanga (2009).

3. Yanga 3-1 Simba Penati (2010)- Penati za Yanga zilifungwa na Godfrey Bony, Stephano Mwasika na Isack Boakye huku penati pekee ya Simba ikafungwa na Mohamed Banka. Wachezaji Emanuel Okwi ,Uhuru Selemani na Said Nyosso walikosa penati kwa upande wa Simba.

4. Simba 2-0 Yanga (2011) Mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Moshi 'Boban' na Felix Sunzu.

5. Simba 3-2 Azam (2012) Mabao ya Simba yalifungwa na Daniel Akuffor, Emanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto huku ya Azam yakifungwa na John Bocco na Kipre Tchetche.

6. Yanga 1-0 Azam (2013) Bao pekee la Yanga lilifungwa na Salum Telela.

7. Yanga 3-0 Azam (2014) Mabao ya Yanga yalifungwa na Geilson Santos 'Jaja' mawili na Saimon Msuva.

8. Yanga 8-7 Azam Penati (2015) Penati za Yanga zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Geofrey Mwashiuya,Thabani Kamusoko,Mbuyu Twite na Kelvin Yondani. Penati za Azam zilifungwa na Kipre Tchetche, John Bocco,Himid Mao,Agrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza,Erasto Nyoni na Shomari Kapombe.

9. Azam 4-1 Yanga (2016) Baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2 muda wa kawaida kwa mabao yaliyofungwa na Donald Ngoma (mawili) kwa upande wa Yanga na Shomari kapombe na John Bocco kwa upande wa Azam ndipo mikwaju ya Penati kwa upande wa Azam ikafungwa na Shomari Kapombe, Michael Balou, Himid Mao, na John Bocco na huku penati pekee kwa Yanga ikifungwa na Deogratius Munishi 'Dida'

Kwa ujumla Yanga imecheza mechi 8 za Ngao ya Jamii na kutwaa Mara 5. Simba imecheza Mara 4 na kutwaa Mara 2. Azam imecheza mara 5 na kutwaa Mara 1, huku Mtibwa Sugar ikicheza mecheza mara 1 na kutwaa mara 1
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’