Nyika awaasa Simba wasiende na matokeo uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2018
Nyika awaasa Simba wasiende na matokeo uwanjani
Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu, unapigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 11 jioni.

Yanga iliyokuwa imeweka kambi mkoani Morogoro tayari imerejea Dar es salaam tayari kwa mchezo huo.

Benchi la Ufundi la Yanga linaloongozwa na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera limesema kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kiko tayari kwa mchezo huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika amesema wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu kwa kila timu kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo.

Hata hivyo Nyika amesema wamejiandaa kikamilifu na amewatahadharisha mashabiki wa Simba wasijaribu kwenda uwanjani na matokeo yao mfukoni.

"Tunawasihi wapinzani wetu wasije na matokeo yao mfukoni kuepusha majangwa yaliyotokea misimu miwili iliyopita"

"Hatupendi waon'goe viti tena kwani tukio hilo litaitia hasara serikali yetu kwa sababu zile kodi zetu za wananchi ndiyo zimejenga uwanjani, hivyo waje kupambana tu uwanjani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’