Stars yaingia kambini leo kuiwinda Cape Verde

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
1 Oct 2018
Stars yaingia kambini leo kuiwinda Cape Verde
Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaanza rasmi leo kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde.

Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.

Mazoezi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park,MNAZI Mmoja.

Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi.

Madaktari Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya

Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa.

Kikosi kilichoitwa

Aishi Manula (Simba)
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Frank Domayo(Azam FC)
Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC)
Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Young Africans)
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Andrew Vicent (Young Africans )
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya zaydi(Azam FC)
Kelvin Yondan (Young Africans)
Paul Ngalema (Lipuli)
Jonas Mkude (Simba)
John Boko (Simba)
Shomari Kapombe (Simba)
Feisal Salum (Young Africans)
Abdallah Kheri (Azam FC)

Wakati huo huo, Bodi ya ligi imefuta michezo mitatu, mchezo namba 83 kati ya Simba Sc dhidi ya African Lyon uliokuwa ufanyike october 06, mchezo namba 87 kati ya Yanga dhidi ya Mbao Fc na ule mchezo namba 90 kati ya Azam Fc dhidi ya Coastal Union kutokana na kuanza kwa kambi ya Timu ya Taifa kujiandaa na michezo miwili ya Kufuzu kwa Afcon 2019 dhidi ya Cape Verde.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →