Zahera ataka Ajib apewe mkataba mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2018
Zahera ataka Ajib apewe mkataba mpya
Ibrahim Ajib amehusika katika mabao sita kati ya 9 ya Yanga msimu huu na hakuna shaka amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga.

Jambo hilo limemfanya Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kuagiza apewe mkataba mpya haraka.

Zahera anafahamu kuwa, Ajibu mkataba wake unaelekea ukingoni na kwa kutambua kuwa jamaa ni bonge la mchezaji, amewaagiza mabosi wa Jangwani kufanya kila njia ili wampe mkataba mpya kabla aliokuwa nao haujaisha kabisa.

Zahera ameliambia gazeti la Mwanaspoti licha ya Ajibu kutofanya vizuri kama alivyotarajia katika pambano la watani, haipotezi maana kuwa mshambuliaji huyo ni moja kati ya mtu hatari aliyenaye katika kikosi chake.

Zahera alisema bado anamhitaji sana Ajibu katika kikosi chake na kwamba anatambua mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu ana anataka abaki hapo.

Mkongomani huyo alisema tayari ameshawaambia mabosi wake kwamba wanatakiwa kuanza mapema mazungumzo ya kumuongeza mkataba mshambuliaji huyo kutokana na kuna vitu anavitaka kutoka kwake kuipa Yanga makali.

Alisema hazitakuwa taarifa nzuri kwake kusikia Ajibu amechukuliwa na timu pinzani ambapo kuhusu mapungufu yake ataendelea kuyafanyia kazi taratibu.

"Nimewaambia viongozi kwamba mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu wanatakiwa wasisubiri mpaka umalizike wanatakiwa kumuongezea mwingine.

"Niseme wazi sitafurahi kusikia Ajibu amechukuliwa na timu nyingine kuna mambo nataka kuyabadilisha hapa na Ajib ni mmoja ya watu ninaowahitaji katika timu yangu," alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’