Ngoma bado ni mchezaji wetu - Mkwassa

Admin By Admin
•
7 Jun 2017
Ngoma bado ni mchezaji wetu - Mkwassa
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwassa amezungumzia hatma ya mshambuliaji wa klabu hiyo Donald Ngoma ambaye anahusishwa kutimka Jangwani.

Mkwasa amesema Ngoma bado ni mchezaji wa Yanga na amemuaga anakwenda kutibiwa huku Mkwasa akiongeza kwamba bado hawajapokea ofa kutoka klabu yoyote kuhusu kumtaka Ngoma.

“Suala lake lina zungumzika vizuri tu, bado anamajeruhi na ameniomba ruhusa anakwenda kupata matibabu lakini bado tupo naye na anapenda bado awe na sisi lakini ana suala lake kubwa ambalo linamsimu kama unakumbuka muda mrefu hajacheza kutokana na maumivu yanayomkabili.”

“Amekwenda kwa ajili ya ‘deep treatment’ kwa hiyo atakapokuwa amepona tutakuwa nae, kwa mujibu wa mkataba bado ni mchezaji wa Yanga kwa sababu hatujapata ofa kutoka sehemu yoyote na tunachofahamu sisi ni kwamba anaendelea na matibabu kwa hiyo hatuwezi kusema chochote.”

Ngoma hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara huku kukiwa taarifa ambazo si rasmi zikidai kwamba mchezaji huyo anaweza kuihama Yanga na kwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3m ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
42m ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →