Zahera awatahadharisha wachezaji wavivu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2018
Zahera awatahadharisha wachezaji wavivu Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera yuko kwao DR Congo akitimiza majukumu ya timu ya Taifa, yeye akiwa kocha Msaidizi wa timu hiyo inayosaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019 kama ilivyo kwa timu yetu ya Tanzania.

Licha ya kutokuwepo nchini, Kocha huyo ameendelea kufuatia kila kinachoendelea kwenye kikosi chake kuanzia mazoezi na mienendo ya wachezaji wake.

Moja ya mambo aliyoyatilia mkazo Zahera tangu atue Yanga ni nidhamu ya wachezaji. Zahera amekuwa mkali kwa wachezaji ambao wanapuuza maagizo wanayopewa.

Tayati imeshuhudiwa baadhi ya wachezaji wakisimamishwa huku wengine wakikatwa mishahara baada ya kukosa mazoezi bila ya kutoa sababu za msingi.

Wakati anaondoka siku chache zilizopita, Zahera alisema aliaandaa program ya mazoezi kwa kipindi chote ambacho hatakuwepo na alimuachia kocha msaidizi, Noel Mwandila.

Zahera alisisitiza kuwa ataendelea kufuatilia kila kinachoendelea kwenye kikosi chake.

"Ninaondoka, na kwenda timu ya Taifa ya Congo lakini nimeacha programu ya mazoezi yote kulingana na udhaifu ulioonekana katika mechi za nyuma, itafanyika kila siku hadi Oktoba 16, ninachotaka ni kila mchezaji kufika mazoezini bila visingizio.

β€œKama kawaida yangu, nitakuwa nafuatilia programu inavyokwenda, mchezaji mvivu na anayetega mazoezini hatacheza mechi hata ikiwa ni ya kirafiki, nitaangalia wale wanaojituma tu,” alisema Zahera.

Leo saa moja jioni Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na Mbao FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara bila ya kocha huyo aliyejipambanua kwa uwazi na ukweli.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’