Makambo, Ajib kuiongoza Yanga dhidi ya Mbao Fc leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2018
Makambo, Ajib kuiongoza Yanga dhidi ya Mbao Fc leo
Kikosi cha Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara, raundi ya tisa.

Yanga itakuwa inashuka dimbani kwa mara ya sita msimu huu, ikiwa imecheza michezo michache zaidi sambamba na Biashara United ya Mara.

Imejikusanyia alama 13 ikiwa imeshinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja dhidi ya Simba Jumapili iliyopita.

Itakuwa inasaka ushindi wake wa tano msimu huu.

Hakuna shaka Yanga itakayocheza na Mbao leo itakuwa tofauti kabisa na ile iliyocheza na Simba wiki iliyopita.

Mchezo dhidi ya Simba, Yanga ilicheza kwa tahadhari zaidi huku ikitumia mashambulizi ya kushitukiza lakini leo Mbao watakutana na Yanga nyingine kabisa.

Nyota Ibrahim Ajib na Heritier Makambo wanatarajiwa kukiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo huo.

Ajib ndio 'engine' ya Yanga wakati huu akiwa amehusika kwenye mabao sita kati ya tisa yaliyofungwa na Yanga.

Amefunga moja na kutengeneza matano.

Makambo na Amissi Tambwe ndio wanaongoza kwa mabao kwenye kikosi cha Yanga wakiwa wamefunga mabao manne, kila mmoja akifunga mabao mawili.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa moja kamili jioni huku viingilio vikiwa; VIP A 15,000/-, VIP B 10,000/-, mzunguko 5000/-
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’